• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 10:50 AM
Sababu za dadake Cohen kukosa mazishi zafichuka

Sababu za dadake Cohen kukosa mazishi zafichuka

RICHARD MUNGUTI na MARY WAMBUI

DADAKE bilionea Tob Cohen, Gabrielle hakuhudhuria mazishi ya ndugu yake kwa vile hakutaka kushiriki katika zoezi hilo na mkewe marehemu anayeshtakiwa kumuua, wakili wa familia alisema.

Bw Cliff Ombeta aliambia Taifa Leo katika mahojiano maalum kwamba ilibidi Gabrielle asafiri Jumamosi ili asijumuike katika maziko ya nduguye na mkewe Sarah Wairimu Kamotho anayezuiliwa katika gereza la wanawake la Langata Nairobi.

“Gabrielle hakutaka kujumuika pamoja na mkewe Cohen katika hafla ya mazishi yake katika makaburi ya Wayahudi mjini Nairobi,” alisema Bw Ombeta.

Alisema Gabrielle aliwaagiza wahudhurie sherehe za kumzisha nduguye kisha watanukuu chochote ambacho kingeendelea katika zoezi hilo wamweleze baadaye.

Ni watu wa familia ya Cohen pekee walioruhusiwa kuingia katika eneo la kufanyia tambiko za kiyaudi za kuwazika wafu katika makaburi ya Wayahudi jijini Nairobi.

Jaji Stellah Mutuku jana aliamuru maafisa wa idara ya magereza wamsindikize Bi Wairimu ahudhurie mazishi ya mumewe.

Mazishi yalianza mwendo wa saa saba mchana na watu kadhaa wakaonekana wakiandaa mazishi, lakini yakasitishwa ghafla iliposemekana hapakuwa na viongozi wa dini wa kutosha kuendeleza shughuli hiyo.

Miongoni mwa waliokuwa wamewasili makaburini ni kakake marehemu, Bw Bernard Cohen.

Ilisemekana waandalizi walifanikiwa kupata Rabbi wanane pekee ilhali walihitaji kumi na hivyo basi mazishi ikaahirishwa hadi leo, saa nane unusu mchana.

Ndugu ya marehemu aliyesalia nchini ndiye alipangiwa kuongoza mazishi hiyo pamoja na kufanya matambiko ya kiyahudi mazishini pamoja na wakuu wa hekalu iliyoko Nairobi.

Cohen, aliyekuwa raia wa Uholanzi na mmiliki wa makampuni kadhaa nchini Kenya aliripotiwa kutoweka na mkewe Sarah mnamo Julai 19 na 20 kutoka nyumbani kwake Kitsuru.

Maiti yake ilipatikana ndani ya tangi la maji lililochimbwa ardhini katika makazi yake ya kifahari yaliyoko Kitsuru baada ya siku 58 tangu alipotoweka.

Korti ilikuwa imeagiza Bi Wairimu afanyiwe uchunguzi wa kimatibabu kiakili kabla ya kusomewa mashtaka.

You can share this post!

Vijana walioiba viti vya Ruto wanyakwa

Hofu HIV kuongezeka wakazi kukataa kondomu

adminleo