Habari Mseto

Seremala aliyemuua mkewe azuiliwa zaidi

October 16th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA VITALIS KIMUTAI

SEREMALA ambaye alimuua mkewe aliyekuwa mwalimu wa shule ya msingi kwa kumwagilia petroli na kumchoma Kaunti ya Bomet atazuiliwa kwa siku siku 10 zaidi kabla ya  kufikishwa kortini.

Bw Robert Kipkorir Tonui amekuwa mafichoni kwa wiki moja na hakujibu mashtaka alipofikishwa mbele ya hakimu wa Sotik Evans Muleka Jumatanno siku moja baada ya kukamatwa kwake.

Wakili wa serikali Mercy Nyaroito aliomba mshukiwa huyo  kuzuiliwa kwa muda zaidi akingoja kufukishwa kortini Oktoba 26,2020.

Bi Nyaroito alisema kwamba mshukiwa huyo kwanzaatafanyiwa vipimo vya kiakili  ambavyo vitasaidia polisi kupata ushaidi Zaidi.

Bw Tonui alisemekana kumchoma mweke EEmmy Chepkoech Mitey aliyekuwa naibu wa mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Cheptalal eneo bunge la Konoin.

Mwathiriwa huyo alikimbizwa hospitali ya Litein kaunti jirani ya Kericho na baadaye kupelekwa hospitali ya Tenwek  ambapo alifariki.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA