• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Serikali kununua treni 18 za abiria kufikia 2019

Serikali kununua treni 18 za abiria kufikia 2019

Na BERNARDINE MUTANU

Serikali inalenga kununua magari ya moshi 18 ya uchukuzi wa abiria na bidhaa kabla ya mwisho wa 2019.

Ripoti hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Uchukuzi James Macharia. Alikuwa akiongea wakati wa mkutano wa kiuchumi kati ya Kenya na China uliofanyika Nairobi.

Wakati wa mkutano huo, China iliahidi kuisaidia Kenya kutekeleza ajenda yake ya maendeleo.

“Kufikia mwishoni mwa Juni, tuna mpango wa kupata magari sita ya moshi. Kufikia mwishoni mwa Desemba 2018, tunaazimia kupata magari 18 kutusaidia kuimarisha biashara,” alisema Bw Macharia.

Kufikia sasa Shirika la Uchukuzi la Reli lina magari manne, moja kutoka mwaka wa 2017 ambalo husafirisha abiria kati ya Nairobi na Mobasa.

Magari ya uchukuzi wa bidhaa huchukua kontena 432 kila siku. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kuhusu Uchukuzi alisema lengo kuu lilikuwani kuchukua kontena 630 kila siku katika muda wa miezi miwili ijayo.

You can share this post!

Miradi ya Ajenda Nne Kuu kuongeza mikopo kutoka Uchina

Jadi Achode achaguliwa kinara wa Mahakama Kuu

adminleo