Serikali yaanza kusaka mafuta na gesi Kajiado
Na BERNARDINE MUTANU
Serikali imeanza shughuli ya kutafuta mafuta na gesi Kajiado. Hii ni kutokana na kuwa kumekuwa na dalili za kuwepo kwa rasilimali hizo eneo hilo.
Kampuni ya Kitaifa ya Mafuta (Nock) inalenga kuchimba bloku yake ya mafuta katika muda wa miaka miwili ijayo, kwa kufuata nyayo za Tullow, kampuni ya mafuta kutoka Uingereza.
Tullow ilipata mapipa karibu bilioni moja katika bloku 10BB na 13T eneo la Turkana Kusini.
Tangu Aprili 2018, kumekuwa na majaribio ya kutafuta mafuta katika Kisiwa cha Pate, Pwani.
Zarara Oil and Gas, kampuni ichunguzayo uwepo wa mafuta wiki hii ilitangaza kuwa haikupata gesi bora inayoweza kuuzwa katika bloku L4 na L13.
Nock, ambaye imekuwa kwa biashara ya mafuta isiyo ghali inalenga kutafuta mshirika na kutoa pesa katika uchimbaji kwa kima kisichojulikana katika Bloku 14T.
“Kuchimba visima vya mafuta ni ghali sana. Kwa kuongeza, ni biashara iliyo hatari kwa sababu unaweza kupata mafuta au gesi au ukose chochote,” alisema mkurugenzi mkuu wa NOCK MaryJane Mwangi.
Kulingana na NOCK, uchunguzi wake ikishirikiana na kampuni ya Japan Oil and Gas Metals Company ulionyesha kuwa huenda bloku hiyo ina mafuta.
Bloku hiyo inaenda kilomita 7,000 mraba na inaenda hadi kwa mpaka wa Tanzania na kampuni hizo mbili zimekuwa zikishirikiana kugharamia uchunguzi huo.