• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 10:50 AM
Serikali yahimizwa kuweka mikakati bora shuleni

Serikali yahimizwa kuweka mikakati bora shuleni

Na LAWRENCE ONGARO

HUKU wanafunzi kote nchini wakijiandaa kurejea shuleni Januari 4, 2021, serikali ni sharti iweke mikakati ifaayo.

Mbunge wa Thika Bw Patrick ‘ Jungle’ Wainaina, alisema maradhi ya Covid-19 ni hatari ndio lakini “hatuwezi kuendelea kuwaweka wanafunzi nyumbani.”

“Jambo muhimu kwa sasa ni wakuu wa shule kote nchini wawe mstari wa mbele kufanya matayarisho kabambe ili wanafunzi wakirejea masomoni kuwe na mpangilio maalum,” alisema Bw Wainaina.

Alisema cha muhimu kwa sasa ni kuwe na vituo vingi shuleni vya kunawa mikono, na kila mwanafunzi awe na barakoa angalau mbili, huku pia kila mmoja akiwa tayari kuweka nafasi ya mita moja hivi kutoka kwa mwenzake.

Aliyasema hayo mnamo Jmanne katika shule ya msingi ya Mugumoini mjini Thika alipokabidhi hundi ya Sh10,000 milioni, kwa wanafunzi wa shule za upili kama basari kupitia walimu wakuu.

Baadhi ya wanafunzi watakaonufaika na fedha hizo wanatoka katika shule za Sekondari ya Broadway, Thika High, Sekondari ya St Paul, Sekondari ya Munyu, Gatuanyaga na Magogoni.

Mbunge huyo alipendekeza wanafunzi wengine wakubaliwe kusomea nje ya madarasa yao iwapo kutatokea msongamano mkubwa madarasani.

Alisema wakuu wa shule watalazimika pengine kuongeza madarasa mengine maalum ili kukabiliana na Covid-19.

 

  • Tags

You can share this post!

Jinsi ya kutengeneza mabuyu

Benzema afunga mawili na kusaidia Real Madrid kupepeta...