• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Simanzi kwa Kaunti ya Kirinyaga wakazi wakizika wanajeshi wawili kufuatia mkasa wa helikopta

Simanzi kwa Kaunti ya Kirinyaga wakazi wakizika wanajeshi wawili kufuatia mkasa wa helikopta

Na GEORGE MUNENE

MAAFISA wawili wa Jeshi waliofariki wakati helikopta ilipoanguka eneo ya Elgeyo Marakwet watazikwa wiki hii katika Kaunti ya Kirinyaga.

Kulingana na familia zao, marehemu Rose Nyawira na John Kinyua, 38, watazikwa katika vijiji vyao vya Kagio na Kirimunge siku ya Alhamisi na Ijumaa mtawalia.

Wawili hao ni miongoni mwa wanajeshi kumi wa KDF waliofariki katika ajali hiyo mbaya iliyoshtua Wakenya.

Mkubwa wao, Jenerali Francis Ogolla ambaye alifariki pia kwenye mkasa huo tayari ashazikwa nyumbani kwake Kaunti ya Siaya.

Sajini Nyawira atazikwa Alhamisi eneo la Kagio, naye Sajini Mkuu John Kinyua atazikwa katika boma lao Ijumaa.

Familia zimejiandaa kuwapa mazishi ya heshima ambayo yatafanyika kwenye vijiji hivyo.

“Sajini Nyawira atazikwa Alhamisi, anastahili mazishi ya kupendeza,” akasema Peter Wachira Kariuki, babake mwanajeshi huyo wa kike.

Sajini Mkuu John Kinyua naye atapumzishwa katika makazi ya familia yao Ijumaa na maafisa wa ngazi za juu wa jeshi, marafiki na viongozi wanatarajiwa kumpa heshima za mwisho.

Wakati huo huo, viongozi wa kisiasa akiwemo Seneta Kamau Murango wametoa wito kwa uchunguzi wa kina kufanyika kubaini kilichosababisha ajali hiyo ya helikopta.

Walisema ni pigo kubwa kwa kaunti moja kupoteza wanajeshi wawili kwa mpigo haswa wakati ambapo walikuwa kazini kujaribu kutatua tatizo la ukosefu wa usalama Bonde la Ufa.

  • Tags

You can share this post!

Hofu baada ya wanne kujeruhiwa na mifugo kuzikwa kwenye...

Madiwani wasuka tena mpango wa kumtimua Kawira

T L