• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Sitayumbishwa na siasa – Uhuru

Sitayumbishwa na siasa – Uhuru

Na CHARLES WASONGA

RAIS Uhuru Kenyatta amesema kuwa hatayumbishwa na kelele za wanasiasa ambao lengo lao ni kuleta migawanyiko nchini.

Akiongea katika nje ya jumba la KICC alipotoa hatimiliki ya ardhi kwa wakazi wa eneo la Embakasi, Nairobi, Rais alisema haja yake kubwa ni kutoa suluhu kwa matatizo yanayowazonga Wakenya.

“Mimi siku hizi sisemi mengi. Lakini nasoma tu katika magazeti kuhusu wanasiasa ambao wanaongea mengi ambayo hayana manufaa kwa wananchi

“Haja yetu ni kutoa masuluhisho yenye manufaa kwa watu wetu. Siyo kugonganisha vichwa vya wananchi kwa mambo ya ukabila na siasa duni ambazo hazisaidii.

‘Mtanitambua kwa vitendo vyangu lakini siyo kwa kupiga nduru kila siku kama wengine. Kazi mtaiona. Wanaopiga kelele acha waendelee,” Rais Kenyatta akaeleza.

Japo hakumtaja kwa jina, kiongozi wa taifa alionekana kurejelea naibu wake, William Ruto, ambaye amekuwa akitoa taarifa mbalimbali, hadharani na kupitia mitandao ya kijamii, haswa kuhusu suala tata la mfumo wa ugavi wa fedha kwa kaunti.

Mnamo Jumanne, Dkt Ruto alionekana kuelekeza lawama kwa maafisa fulani wa serikali kufuatia kukamatwa kwa maseneta watu Jumatatu siku ambayo walipaswa kuhudhuria kikao cha kujadili suala hilo.

Naibu Rais alionya dhidi ya polisi kutumiwa kuwanyanyasa maseneta hao kutokana kwa misingi ya msimamo wao kuhusu suala hilo, akisema kitendo hicho ni kinyume cha Katiba.

Na mnamo Alhamisi Dkt Ruto aliilaumu serikali kuhusiana sakata ya wizi wa mabilioni ya fedha za kufadhili vita dhidi ya Covid-19 huku akijiondoa lawamani.

“Angalau sitalaumiwa kutoka na wizi wa pesa za Covid-19 kwa sababu inasemekana kuwa nimetengwa. Ni sawa tu,” akasema kupitia Twitter.

Ijumaa Rais Kenyatta aliwaambia wanasiasa kwamba uongozi hutoka kwa Mungu na ni yeye atakayeamua yule atakuwa Rais “wakati huo ukitimu.”

  • Tags

You can share this post!

Mwalimu mwenye mikono ya dhahabu

Mungatana aomba kesi dhidi yake isuluhishwe nje ya mahakama