• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:42 PM
Spika wa zamani aililia kaunti imlipe mamilioni

Spika wa zamani aililia kaunti imlipe mamilioni

NA RUTH MBULA

SPIKA wa zamani wa Bunge la Kaunti ya Kisii Kerosi Ondieki sasa anataka alipwe marupurupu ya zaidi ya Sh2 milioni na bunge hilo.

Bw Ondieki aliyehudumu kwa miaka mitano kutoka 2013 hadi 2017 tayari amepata huduma za wakili kuhakikisha amelipwa fedha hizo.

Katika barua aliyoandikia mwenyekiti wa Bodi ya Huduma ya kaunti hiyo, Bw Ondieki anasema ana haki ya kulipwa marupurupu ya nyumba ya Sh75,000 kila mwezi kwa kipindi cha miaka mitano alichohudumia kaunti hiyo.

“Wakati nikiwa ofisini, nilisafiri Ureno kwa ziara rasmi na nilikuwa nilipwe marupurupu ya Sh890,000, lakini sijalipwa kufikia sasa,” anasema.

Anataka malipo hayo ayapate katika muda wa siku 14, na isipofanyika hivyo amesema atafika mahakamani kupata haki.

Amesema viongozi wenye ushawishi mkubwa katika kaunti hiyo wamekuwa wakuzuilia malipo yake ili kutimiza matakwa yao wenyewe.

“Baadhi ya viongozi wamekuwa wakihujumu mchakato wa bunge kunilipa. Lakini nataka kuwaambia wakome kutumia mamlaka visivyo kuwatesa watu. Nilihudumu vyema kama spika na ninafaa kuheshimiwa,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Kaunti ya Nairobi yazidi kutwaa nafasi za maegesho...

Krismasi ya mapema kampuni ya magari ikiwapuguzia wateja bei

adminleo