Habari Mseto

Taharuki Naivasha jamii zikizozania mifugo

October 21st, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA MACHARIA MWANGI

Taharuki imetanda  eneo la Maai Mahiu, Naivasha baada ya wanakijiji kuchukua ng’ombe 72 wanaomilikiwa na wafugaji wa eneo hilo kama njia moja ya kulipiza kisasi.

Walipelekwa ng’ombe hao kwenye kituo cha polisi cha Maai Mahiu huku wakidai kwamba wataachilia ng’ombe hao baada ya kurudishiwa mbuzi wao walioibwa Jumatatu usiku.

Tukio hilo limeleta taharuki kati ya  jamii hizo mbili huku ikimlazimu naibu Kamishena wa kaunti ya Naivasha Kisilu Mutua kuingililia kati.

Wafungaji hao walisema kwamba ng’ombe 100 waliibwa na si 72, na wanadai kurudishiwa. “Bado tunajaribu kubaini ni ng’ombe wangapi walioibwa na bado uchunguzi unaendelea,” alisema afisa huyo.

Bw Mutua aliwaonya wote waliohusika kwenye kisa hicho kwamba watakamatwa na kupelekwa kortini.

“Tunatafuta watu waliochukua ng’ombe hao kwa lazima na watakamatwwa,” alisema afisa huyo.

Aliwaomba maafisa wa usalama kuangalia maswala ya uhalifu yaliwemo wizi wa mifugo kwani unachangia vita dhidi ya jamii hizo.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA