• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 9:50 AM
Toyota yawapa polisi magari 800 kuimarisha usalama

Toyota yawapa polisi magari 800 kuimarisha usalama

Na PETER MBURU

IDARA ya Polisi imepokea magari 800 kutoka Toyota Kenya kupitia mradi wa serikali ambao unalenga kuimarisha usalama wa taifa na kukabili upungufu kwenye huduma ya kitaifa ya polisi (NPS).

Magari hayo yatakuwa yakiwasili kwa kipindi cha wiki mbili zijazo, yakinuia kuwapa motisha maafisa wa polisi kuchapa kazi vyema.

Mradi huo wa kuinunulia NPS magari ulikamilika mnamo Oktoba 2013, wakati Toyota Kenya ilipata zabuni ya kusambaza magari 1,100.

Ni mradi uliogharimu serikali Sh6 bilioni, huku kikundi cha kwanza cha magari hayo kikiwa kiliwasili nchini Disemba mwaka huo.

Kwa sasa, idara hiyo ina upungufu wa magari 4,500 huku idadi hiyo ikitarajiwa kupanda hadi 11,000 kwa kipindi cha miaka mitano ijayo baada ya afisi zaidi za ukurugenzi kuongezwa, afisi za kikatiba na idara ya upelelezi iliyowezeshwa.

Zaidi ya maafisa 2,500 wa polisi wamefunzwa kuhusu kutumia magari hayo katika kaunti 41, akasema Mkurugenzi Mkuu wa Toyota Kenya Arvinder Reel akasema.

  • Tags

You can share this post!

BEI GHALI: Omtatah afika mahakamani kuokoa Wakenya

COTU pia yaishtaki serikali kuhusu ushuru wa mafuta

adminleo