• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 3:16 PM
TrustAfrica na IEJ zatangaza kongamano nchini Senegal kuangazia masuala ya ustawi kiuchumi na kiutawala barani Afrika

TrustAfrica na IEJ zatangaza kongamano nchini Senegal kuangazia masuala ya ustawi kiuchumi na kiutawala barani Afrika

Na CHRIS ADUNGO

TrustAfrica (TA) na Taasisi ya Haki za Kiuchumi (IEJ) zina furaha ya kutangaza kuandaliwa kwa kongamano la siku tatu kuhusu Udadisi wa Usahihi na Uhalisia wa Fikra za Kiuchumi Barani Afrika: Kutalii Mbinu Mbadala. Kongamano hili linalodhaminiwa na Shirika la Mradi wa Open Society kwa Mataifa ya Afrika Magharibi (OSIWA) litafanyika jijini Dakar, Senegal kati ya Septemba 2-4, 2019.

Bara la Afrika linajivunia utajiri mkubwa wa vipaji na nguvu-kazi kutoka kwa vijana wabunifu, wingi wa mali asili, soko pana la pamoja, uwezekano wa kupanua zaidi viwanda vya ndani na kanzi kubwa ya nguvu-kazi ya kibinadamu ambayo haijatumika ipasavyo.

Ingawa hivyo, bara la Afrika bado lina mataifa 39 yaliyo na kiasi cha juu zaidi cha umaskini na viwango vya chini kabisa vya maendeleo ya kibinadamu.
Japo haiwezekani kuitenganisha hali hii na karne nyingi za kipindi cha ukandamizaji, pia ni zao la njia zilizochukuliwa na kukumbatiwa (kwa kulazimishwa au kwa hiari) na tawala za baada ya uhuru.

Muhimu zaidi ni pupa ya kulazimishia watu miradi mbadala ya kimuundo, sera za Miafaka ya Washington na sera za Miafaka ya Baada ya Washington, na aina mbalimbali ya “mageuzi” huria ya hivi karibuni ambayo yametekelezwa na kuhalalishwa na mielekeo ya kisasa ijulikanayo kama “uhalisia wa kiuchumi”.

Hali hii imesababisha ukawaida wa asasi huria za kimamboleo kuita nyingi za nchi za Kiafrika Mataifa Maskini Yaliyo na Madeni Mazito (HIPC).
Hata hivyo, bara la Afrika lina fursa ya kujibadilisha kwa namna ambayo itainua viwango vya maisha, kuzingatia maslahi pamoja na kuendeleza haki na heshima ya watu wote kwa amani, umoja na uhuru.
Ili kuishughulikia mitanziko hii inayokabili bara letu, ni muhimu tuelewe na tuudadisi usahihi wa uhalisia wa kiuchumi, tubuni mbinu mpya za kuwazia masuala ya kiuchumi na kuipa nguvu mikakati ya kutekeleza mbinu mbadala. Haya ndiyo malengo makuu ya kongamano hili. Madhumuni ya mkutano huu hasa ni:

  • Kuondoa uchukulio wa mawazo ya kawaida ya kiuchumi na miundo ya kisiasa ambayo ilibuniwa kuwezesha kuwepo kwa haya;
  • Kuhoji mitazamo ya kiuchumi ambayo inaweza kuchangia upana wa maendeleo jumuishi na kushughulikia kwa njia faafu zaidi masharti ya haki za kijamii katika muktadha wa Kiafrika;
  • Kuibua mifano mbadala na kutoa fursa pamoja na mazingira salama ya fikra tofauti;
  • Kutalii njia mbalimbali za kuchangia maendeleo na/au kuendeleza mifumo na mielekeo ya kiheterodoksi kuhusu masuala ya kiuchumi miongoni mwa wasomi na wataalamu katika vyuo vikuu vya Afrika; na
  • Kusaidia asasi na makundi ya kiharakati kote Afrika kuendeleza ajenda za utetezi wa haki na udumishaji wa haki ya kiuchumi ili kuchangia maendeleo na utekelezwaji wa haki za kibinadamu.

  • Tags

You can share this post!

KCB, Homeboyz zatinga robo-fainali ya duru ya tano Christie...

MWANASIASA NGANGARI: Kiano: msomi aliyetetea...

adminleo