• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 9:55 AM
UDA: Ruto awatoa mnofu mdomoni maafisa walafi wa pesa za tableti

UDA: Ruto awatoa mnofu mdomoni maafisa walafi wa pesa za tableti

NA MOSES NYAMORI

RAIS William Ruto alizima ununuzi wa tableti 10,000 kwa gharama ya Sh200 milioni zilizonuiwa kutumiwa na chama chake cha UDA katika uchaguzi wa mashinani baada ya kugundua kuwa maafisa wa chama hicho walikuwa wameongeza bei.

Baadhi ya maafisa wa chama walikuwa wameipa zabuni kampuni ya humu nchini kuuza vifaa hivyo kwa bei ya Sh20,250 kila moja. Bei ilikadiriwa kuwa Sh25,000 kwa kila moja kwa kujumuisha ushuru wa ziada wa thamani (VAT).

Hata hivyo Rais Ruto anasemekana kukasirishwa na hatua ya maafisa hao na akaagiza tenda hiyo ifutwe na kupatiwa kampuni nyingine.

Taifa Leo ilibaini kuwa vita kuhusu zabuni hiyo ya Sh200 milioni ndizo zilifanya uchaguzi kuairishwa kutoka Desemba 9, 2023.

Jana, Katibu Mkuu wa UDA Cleophas Malala alikiri kwamba kampuni ya kwanza ilikuwa imetoa bei ya Sh25,000 na kwamba Rais Ruto binafsi alizinunua kutoka China kwa Sh10,125.

  • Tags

You can share this post!

Treni za abiria zasitisha uchukuzi jijini kufuatia mvua...

Ni njia tofauti za upendo au mgawanyiko?

T L