• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Uingereza yatoa fedha kusaidia Wakenya wanaohangaishwa na mafuriko

Uingereza yatoa fedha kusaidia Wakenya wanaohangaishwa na mafuriko

NA NYABOGA KIAGE

SERIKALI ya Uingereza imeipa Kenya Sh140 milioni kukabiliana na athari za mafuriko.

Kwenye taarifa Jumapili, ubalozi wa Uingereza nchini ulisema ufadhili huo utasimamiwa na Hazina ya Watoto ya Shirika la Umoja wa Mataifa  (UNICEF), ili kusaidia jumla ya familia 6,900 kwenye kaunti zilizoathiriwa zaidi na mafuriko.

Kwa mujibu wa ubalozi huo, shirika la UNICEF linatarajiwa kutoa misaada ya dharura ya kiafya, chakula na mahitaji ya usafi kama maji ya kunywa na mazingira salama.

Shirika hilo pia linatarajiwa kutumia pesa hizo kuimarisha mikakati ya kukabili kuzuka au kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu kwenye kambi.

Litahakikisha watu walio mbali na makao yao, wanaishi salama, bila ya kuambukizwa maradhi yanayosababishwa na maji machafu.

Mkurugenzi wa UNICEF nchini, Bi Shaheen Nilofer, alisema wataangazia zaidi usalama wa watoto.

“Kila kunapozuka masuala ya dharura, wanaoathiriwa zaidi huwa watoto. Hao ndio watakaotushughulisha zaidi. Kupitia ubalozi wa Uingereza, tutaweza kutoa msaada wa hali na mali kwa familia za watoto walioathiriwa zaidi,” akasema Bi Nilofer.

  • Tags

You can share this post!

Raila achomoa kucha na kushambulia serikali baada ya kimya...

Liverpool, Chelsea wafufuka muda ukiyoyoma huku Spurs...

T L