Habari Mseto

Ukaguzi mkali Mashujaa Dei Kisii

October 20th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA RUTH MBULA

Mamia ya wananchi wa Kisii waliamka asubuhi na mapema kufika kwenye uwanja wa Gusii mapema Jumanne huku ukaguzi mkali ukifanyika kama njia moja ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kufika kwenye uwanja huo kwa sherehe za Mashujaa Dei zinazofuatia baada ya miezi ya matayarisho na kaunti hiyo ya Kisii.

Saa kumi na mbili asubuhi wakazi wa Kisii walikuwa wamepanga poleni refu zilizozimehukua kilomita kadhaawakiwa tayari kuhudhuria mkutano huo.

Watu hao kwanza walikuwa wanakaguliwa kwanza na kupimwa joto kabla ya kurusiwa kuingia ndani.Saa moja na nusu ni watu wachache waaliokuwa tayari wameruhusiwa kuingia kuingia ndani ya uwanja.

Kaunti ya Kisii imekuwa ikijitayarisha kwa siku nyingi kwa sherehe hiyo. Usiku wa Jumatatu maafisa wa GSU walifanya ukaguzi kuakikisha kwamba usalama umeimarishwa.

Barabara zote za Kisii zilibakia mahame kwani magari yote yalizuiliwa kufika ndani ya mji wa Kisii.

Kaunti ya Kisii anandaa sherehe za mwaka huu kama mpango waa serikali kuandaa sherhee hizo nje ya Nairobi  n ani watu 4,000 pekee wanao ruhusiwa kuingia ndani ya uwanja wa Gusii ili kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

Zaidi ya watu 8,000 watakuwa wakiona sherehe hizo kutoka kwa televisheni iloyowekwa kwenye mji wa Kisii.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA