Habari Mseto

Ukosefu wa ukaguzi wa kina mpakani Busia waibua hofu

May 26th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA CAROLINE WAFULA

Hofu imezuka baada ya kubainika kwamba ukosefu wa ukaguzi wa watu katika mpaka wa Busia umepelekea watu wawili waliokuwa na virusi vya corona kuingia humu nchini majuzi.

Wawili hao walikamatwa jijini Kisumu saa chahe baada ya matokeo ya yao ya Covid-19 kuoyesha kuwa walikuwa na virusi hivyo.

Maelezo zaidi yanasema kuwa wawili hao ni madereva wa masafa marefu wa miaka 29 na 82 walioingia nchini kutoka Sudan Kusini na Uganda kupitia mpaka wa Busia.

Ni wazi kwamba waliruhusiwa kuingia humu nchini kabla ya kupokea matokeo yao ya vipimo vya virusi hivyo.

Walipatikata Kisumu na kulazimishwa kuwekwa kwa karatanti katika Hospitali ya Jaramogi.

Kesi ya tatu katika kaunti hiyo hivi majuzi ni ya mwanamke wa miaka 33 aliyetoka Nairobi hadi Nyando kuhudhuria mazishi Jumatano na kurudi tena Nairobi.

Alikuwa mmoja wa waombolezaji 20 waliopimwa na kukwekwa karantini. Kulingana na Gavana Anyang Nyongo waliotangamana na madereva hao wanaendelea kutafutwa.