• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
‘Upandaji mbegu’ kanisani uzimwe, asema kasisi

‘Upandaji mbegu’ kanisani uzimwe, asema kasisi

Na SAMMY KIMATU

KASISI mmoja jijini Nairobi ameunga mkono kukaguliwa kwa makanisa baada ya kushuhudiwa kwa ongezeko la makanisa nchini yanayowatapeli waumini kwa jina la Mwenyezi Mungu na kuwaambia ‘wapande mbegu’.

Kasisi huyo aliongeza kwamba wahubiri husika wana ‘nguvu’ za kuwanasa watu badala ya kutumia nguvu za kiroho.

Reverend Sammy Kibira ,42, wa kanisa la Pentecostal Assemblies of God (PAG) mtaani wa mabanda wa Mukuru-Kaiyaba, South B alisema wahubiri hao hawana mafunzo ta kithiolojia sawia na mfunzo ya usimamizi wa uongozi.

“Nawauliza wananchi kuwa macho. Chunguzeni taarifa za Imani, eleweni Imani ya kanisa lenyewe na mhunguze misingi yake kabla hamjajiunga nalo,” Kasisi Kibira akasema.

Kadhalika, Kasisi Kibira aliongeza kwamba makanisa nia lazima yafanyiwe uhasibu na kuwaomba wananchi kujinga na makanisa yaliyojikita kimafunzo ya biblia takatifu bhadala ya kupotoshwa na kuitishwa ‘kupanda mbegu.”

Aliongea hayo alipokuwa akiongoza ibada ya Jumapili.

  • Tags

You can share this post!

Watafunaji miraa walalamikia kodi ya juu

Kizimbani kwa kumtupia manamke jicho la mapenzi kwa baa

adminleo