Upinzani wawazia kuondoa baadhi ya wawaniaji Malava kama mkakati dhidi ya serikali
BAADA ya muafaka kufikiwa na upinzani kuamua kuwasilisha mwaniaji moja kwenye uchaguzi mdogo wa Mbeere Kaskazini, juhudi hizo sasa zinaeendelezwa eneobunge la Malava Kaunti ya Kakamega.
Katibu Mkuu wa DAP-K Eseli Simiyu amefichua kuwa mazungumzo yanaendelea ili waachiwe kiti hicho na waungwe mkono na vinara wengine wa upinzani.
Mbali na DAP-K kumsimamisha Seth Panyako, DCP inayoongozwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua imekuwa ikiendeleza kampeni kali kwa mwaniaji wake Edgar Busiega.
“Kutakuwa na mwaniaji mmoja wa upinzani jinsi tu ilivyo Mbeere Kaskazini na tunaendelea kushauriana kuhusu hili,” akasema Bw Eseli.
“Kile ambacho tutafanya ni kubaini nani ni maarufu ili tusiwasimamishe wagombeaji wawili tofauti na kunufaisha UDA,” akasema Dkt Eseli.