• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 3:46 PM
Vijana Thika washauriwa kukumbatia kilimo cha macadamia

Vijana Thika washauriwa kukumbatia kilimo cha macadamia

Na LAWRENCE ONGARO

VIJANA wamehimizwa kuwa wabunifu ili kujiajiri wenyewe badala ya kutegemea ajira kutoka kwa serikali.

Mbunge wa Thika Bw Patrick ‘Jungle’ Wainaina amewashauri vijana kuzinduka walipo na kuanza kujitegemea pakubwa kwa kubuni ajira; hasa mashinani.

Katika eneo la Kilimambogo, Thika Mashariki, kikundi cha vijana wapatao 15 kimeitikia mwito huo na tayari wameanza upanzi wa zao la Macadamia.

“Ninafurahia mwelekeo uliochukuliwa na kikundi hiki cha kujitegemea wenyewe ili kujitafutia riziki siku za usoni,” alisema Bw Wainaina.

Mwishoni mwa wiki jana mbunge huyo alizuru Kilimambogo ili kujionea mwenyewe kazi njema ya kilimo kinachofanywa na kikundi hicho ambacho kimeasi upanzi wa mahindi, na maharage na badala yake kukumbatia zao la Macadamia.

Mche wa macadamia. Picha/ Lawrence Ongaro

“Mimi ndiye nilichukua jukumu la kukihamasisha kikundi hicho ambacho kimekuwa kikiwazia ni zao lipi linaloweza kukuza kujinufaisha katika kilimo,” akasema.

Alisema yeye kama mjuzi wa zao hilo aliona ni vyema wazamie katika kilimo hicho ili baada ya miezi kadha wawe wanaweza kuvuna kitita kizuri cha pesa.

Alisema kikundi hicho kimefanya vyema kwa sababu kinaambatanisha maono yao na ajenda nne muhimu za serikali ambapo moja baina ya hizo ni ajira.

Mazao mazuri

Alisema atafanya juhudi kuona ya kwamba kikundi hicho kinapata ufadhili wa fedha za Uwezo Fund ili vijana waweze kuharakisha uwezo wao wa kupata mazao mazuri.

Kiongozi wa kikundi hicho, Bw Peter Maina Mburu alisema walizindua mpango huo miezi sita iliyopita ambapo walipanda miche 500 ya Macadamia na tayari wamejiandikisha rasmi kama kikundi.

“Mara ya kwanza kuzindua mradi huo ilikuwa ni kibarua kikubwa kuwajulisha vijana umuhimu wa mpango huo. Lakini baadaye walipata ukweli wa mambo na kuamini uzuri wake,” alisema Bw Mburu.

Alisema kikundi chao kilipewa ushauri wa kufana katika kampuni kubwa ya matunda ya Macadamia ya Bob Hariss mjini Thika.

Alisema ana matumaini makubwa ya kwamba zao hilo litakapokomaa vilivyo watanufaika pakubwa ambapo kila mmoja atakuwa na pesa mfukoni.

“Tayari tuna shamba lenye ukubwa wa ekari moja hapa Kilimambogo ambapo jambo muhimu kwa sasa ni kunyunyizia mimea hiyo maji.

You can share this post!

Kamworor azoa Sh2.8 milioni baada ya kuvunja rekodi

KCB yachupia kilele cha ligi baada ya sare

adminleo