• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 8:46 PM
Viongozi wakashifu mauaji ya polisi na utovu wa usalama Isiolo

Viongozi wakashifu mauaji ya polisi na utovu wa usalama Isiolo

VIVIAN CHEBET na LUCY KILALO

VIONGOZI wa kaunti ya Isiolo wameshtumu vikali mashambulizi ambayo yamesababisha vifo vya polisi watatu na kuwajeruhi wengine sita mwezi Juni pekee.

Viongozi hao sasa wanataka serikali kuendesha operesheni ya kuchukua silaha haramu miongoni mwa wakazi.

Mbunge wa Isiolo Kaskazini Hassan Hulufo, alisema kuwa serikali inastahili kuchukua hatua kali dhidi ya wavamizi hao.

“Nani yuko salama ikiwa kamanda wa usalama hayuko salama?” aliuliza huku akimtaka Waziri wa Usalama Fred Matiang’i kuchukua hatua kali.

Majangili waliwaua maafisa watatu wa polisi na kuwajeruhi wengine sita mwezi huu pekee katika operesheni iliyokosa kufaulu ya kuwarejesha mifugo iliyoibwa.

Jumatatu jioni, polisi wawili walipigwa risasi na majangili katika maeneo ya Nachuroi na Ngaramera huku wengine sita akiwemo kamanda mkuu wa polisi katika kaunti Isiolo Manase Musyoka wakinusurika na kupata majeraha mabaya ya risasi.

Jumanne, viongozi hao walisema kuwa Bw Manase angali amelazwa ingawaje ametolewa kutoka kwa chumba cha wagonjwa mahututi.

Mnamo Juni 6, afisa wa polisi alipigwa risasi katika eneo la Chumvi kata ya Ngaremara kwenye uvamizi wa kushtukiza na majangili walipokuwa katika operesheni ya kutafuta mifugo iliyoibwa katika kijiji cha Loruko mwezi uliopita.

Juhudi za serikali za kupata mifugo hiyo hazijazaa matunda ingawa maafisa wakuu wa usalama wametekeleza operesheni mbili kubwa katika eneo hilo.

Kamishina wa kaunti ya Isiolo John Ondego aliyethibitisha uvamizi huo alisema maafisa wake walimiminiwa risasi walipokuwa wakiiweka mifugo waliyoipata ndani ya lori.

“Majangili hao walijiweka vizuri katika maeneo ya juu kuwalinda mifugo waliokuwa katika maeneo ya chini. Hapo ndipo walivamiwa na ufyatulianaji wa risasi ukasababisha kifo cha afisa moja wa polisi,” akasema Bw Ondego.

Makabiliano hayo makali yalipelekea polisi kujiondoa na majangili hao wakachukua usukani na kutwaa mifugo hiyo.

Wakihutubia wanahabari nje ya majengo ya bunge, pia waliitaka serikali kuendesha harakati za kuwasaka majangili bila kuhangaisha abiria njiani.

“Abiria wanahangaishwa barabarani ilhali wavamizi wanajulikana. Acheni kuhangaisha abiria ambao wanasafiri kwa amani,” alisema mbunge wa Moyale, Bw Gufu Wario akieleza kuhusu alichoshuhudia njiani akija Nairobi.

baada ya tukio hilo,” Wario alieleza.Viongozi hao ambao walikuwa ni pamoja na Mwakilishi Mwanamke wa Kaunti ya Isiolo Rehema Jaldesa na mwenzake wa Marsabit Safia Adan, walitaka matukio hayo ya uvamizi kukomeshwa ili kuzuia uchumi wa eneo hilo kusambaratika.

You can share this post!

Wasiwasi mpya wa mgawanyiko wazuka Jubilee

Aliyechaguliwa kwa ODM atangaza kuwania kwa Jubilee 2022

adminleo