Habari Mseto

Waandamana kulalamikia kusitishwa kwa ujenzi wa barabara

September 28th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA CHARLES LWANGA

Wakazi wa Malindi wameandaa maandamano ya kulalamikia kusimamishwa kwa ujenzi wa barabara inayofadhiliwa na Benki ya Dunia inayogharimu Sh67 milioni eneo la Mtangani, Kaunti ya Kilifi.

Wakazi hao wakiongozwa na madiwani Kadenge Mwathethe (Shela),  Edward Kazungu Dele (Sabaki) na David Kadenge Dadu (Malindi mjini), walisema kwamba walishangazwa na jumuiya ya wafanyabiashara wakazi wa Malindi ambao walienda kortini ili kuzuia kujengwa kwa barabara hiyo.

“Jumuiya hiyo ya wanabiashara walioenda kortini ili kuomba kusimamishwa kwa ujenzi wa barabara hiyo hawana haja na maitaji ya  wananchi ,”alisema bw Kadenge wananchi wamekuwa wakigoja barabara hiyo kwa miaka mingi kwa  watu wachache kusimamisha mradi huo”.

Hii ni baaada ya Jumjiya ya wafanyabiashara ikiogozwa na kikundi cha Malindi Progressive wwlfare Assocatio Pamoja na KNCCI walienda kortini kusimamisha ujeenzi wa barabara hiyo.