• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 5:50 AM
Waandamana mwenzao aliyeuawa na polisi akizikwa

Waandamana mwenzao aliyeuawa na polisi akizikwa

NA CHARLES WANYORO

Mwanamume wa miaka 19 aliyesemekana kupigwa hadi kifo na maafisa wa polisi alizikwa kwenye Kijiji cha Antuathama, Kaunti ya Meru Jumatano.

Mamia ya waombolezaji wakiwemo waendesha bodaboda walifanya maandamano ya usalama mjini Maua kelekea kanisani Amung’enti ambapo misa ya wafu ya Spencer Thuranira ilifanyika.

Viogozi wa kaunti ya Meru wakiogozwa na waziri wa Rufus Miriti, mwenyekiti wa chama cha ODM Jacob Munoru Pamoja na  Mithika Mwenda mkurugenzi wa  Pan-Africa Climate Justice Alliance walitaka uchunguzi ufanyike kwa haraka.

Viogozi hao walisema kwamba kijanahuyo amabye alifanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana na kujizolea alama ya B+ alikuwa akisafiri  kwenda Maua kununua dawa za mamayake wakati bodaboda liyokuwa amepanda lilisimamishwa na polisi hap ndipo polisi walianza kumpiga Spencer ambaye alifariki baadaye..

Kulingana na upasuaji Spencer alifariki kutokana na majeraha kichwani.

Bw Miriti alijutia kifo cha kijana huyo huku akisema kwamba kifo hicho kilichukua Maisha ya kijana aliyekuwa na maono ya kuwa engineer..

“Tumechukizwa na na kifo cha ijana huyu natunataka kukemea tunakemea unyama unaotekelezwa na polisi,” walisema maafisa wa kaunti.

  • Tags

You can share this post!

Wapenzi wasema walimuua mtoto kuokoa uhusiano wao

Wito serikali idhibiti maajenti wanaowapeleka Wakenya...