• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 10:01 AM
Waathiriwa wa ghasia za 2007 walia kukosa fidia sikukuu ikianza

Waathiriwa wa ghasia za 2007 walia kukosa fidia sikukuu ikianza

Phylis Musasia Na Mercy Koskey

WAATHIRIWA wa ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007/2008 katika kijiji cha Jogoo, eneo la Kamara, Kaunti ya Nakuru, wamekosoa serikali kwa kuchelewa kuwalipa fidia huku sherehe za sikukuu zikianza.

Kwa miaka mingi sasa, zaidi ya familia 600 katika eneo hilo bado zinaishi katika mazingira duni licha ya serikali kuahidi kutoa misaada ya kushughulikia maslahi yazo.

Kulingana na mwenyekiti wa kundi hilo, David Kahwai, waathiriwa hao walipata usaidizi wa nyumba za muda kutoka kwa baraza la wakimbizi la Denmark ambazo kufikia sasa ziko katika hali mbaya.

Chifu wa eneo hilo, Bw Kuria Mburu alithibitisha kuwa wahasiriwa hao wamekuwepo tangu baada ya ghasia za uchaguzi huo na akasema anatumai serikali itashughulikia matakwa yao.

“Rekodi zao zipo katika afisi za kamishina wa kaunti na ni dhahiri kuwa idadi kamili ya waathiriwa ni familia 670 kutoka eneo la Jogoo,” akasema.

Kulingana naye, mamia ya wahasiriwa wengine wanazidi kuhangaika katika vijiji vya Rironi, Mlima, Total, Karandi, Haraka, Kamkunji, Gitira, Nyakinywa, Baraka, Kagawa na Kiwanja Ndege kwenye eneo la Kamara.

Taifa Leo ilipozuru kijiji cha Jogoo Jumatatu, baadhi ya nyumba zilikuwa na unyevunyevu sakafuni huku sehemu za kuta zikianza kubomoka.

 

  • Tags

You can share this post!

Gavana anukuu Biblia huku akigura kundi la Ruto

Mvua sasa kupungua siku 7 zijazo

adminleo