Wafanyakazi 14 wa Safaricom sasa wana corona
By DAVID MUCHUI
Watu 13 waliopatikana na virusi vya corona Jumatano katika Kaunti ya Meru ni wafanyakazi wa Safaricom wanaofanya kazi katika duka la huduma ya Safaricom mjini Meru.
Visa hivyo vya Jumatano vinafikisha wafanyakazi wa Safaricom waliopatwa na virusi vya corona 14 baada ya mfanyakazi mwingine kupata virusi vya corona Ijumaa wiki iliyopita.
Kulingana na Waziri wa afya wa kaunti ya Meru Misheck Mutuma watu 42 waliotangamana na hao 13 waliotengwa Ijumaa wamewekwa kwenye karantini Jumatano.
“Hao 13 walitangamana na 42 wako karantini.Bado tunaendelea kuwatafuta waliotangamana na hao 13,” alisema Bw Mutuma.
Kufuatia visa hivyo 13 Safaricom walifunga duka lake kwa muda usiojulikana.
Afisa mkuu wa Afya kaunti ya Meru James Kirimi alisema kwamba waendelea kutafuta waliotangama na 13 hao.
“Kati ya hao 13 saba ni wanaume na wanawake sita. Tumejitayarisha kuwashungulikia hao 13 katika Hospitali ya mafunzo ya Meru,” alisema Dkt Karimi.
Kuna watu 15 katika hospitali ya Meru pamoja na dereva wa lori aliyetengwa Mei 26 akiendelea matibabu.