• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:42 PM
Wafungwa walilia ngono

Wafungwa walilia ngono

Na ALEX AMANI

WAFUNGWA wanaotumikia kifungo cha maisha katika gereza la Mtangani eneobunge la Malindi, Kaunti ya Kilifi wameiomba serikali ipitishe sheria itakayowapa haki zao za kimsingi ikiwemo tendo la ndoa kwa waliofunga pingu za maisha.

Akizungumza na wanahabari Jumanne mjini Malindi katika gereza la Mtangani Bi Sofia Swaleh anayetumikia kifungo cha maisha kwenye gereza la wanawake, amesema licha ya kuwa wanatumikia vifungo bado wangali na hisia za kimwili huku akipendekeza kuwe na mpango madhubuti wa wao kukutanishwa na wapenzi wao au wanandoa wenzao.

“Ninataka niwambie hivi japo tunatumikia vifungo gerezani ila pia sisi tunahisia za kimwili tunaiomba serikali ikaweze kubuni mpango utakaotuwezesha sisi kukutana wapenzi wetu ama wanandoa wenzetu ili tupate haki zetu za ndoa,” amesema Bi Sofia.

Hata hivyo Bi Sofia, amesema iwapo swala hilo litaidhinishwa basi ni sharti wana ndoa hao wapimwe virusi vya ukimwi miongoni mwa magonjwa mengine ya zinaa kabla ya kuruhusiwa kuchamiana na wapenzi wao ili kuhakikisha usalama wao wa kiafya.

“Ninasema iwapo jambo hili litaidhinishwa, basi sharti kila mmoja afanyiwe vipimo kwanza kabla ya kuruhusiwa kujamiana ili kuhakikisha usalama wa kiafya,” amesistiza Bi Sofia.

Wakati ou huo Bi Sofia, ameiomba serikali kupitia idara ya magereza kuwapatia fursa ya kutumia ujuzi wanao pata magerezani kuwa kitega uchumi kwao ili kupata fedha za kukimu familia zao licha ya kuwa wanaendeleo kutumikia vifungo.

  • Tags

You can share this post!

JOGOO WA JIJI: Manchester United yaizidi maarifa Manchester...

Askofu ahimiza upendo miongoni mwa wanajamii

adminleo