Waiguru aokoa wafugaji kuku
Na George Munene
Kaunti ya Kirinyaga imewaokoa wafugaji wa kuku ambao wanakumbwa na matatizo ya kukosa chakula bora cha kuku na kwa bei nafuu.
Wakulima wengi wamelazimika kuacha biashara hiyo ya kufuga kuku kwani chakula cha kuku kimekuwa bei ghali huku wanaendeleza wakipata hasara.
Lakini sasa serikali ya gavana Waiguru imeanzisha kiwanda cha kutengeneza chakula cha mifugo ambacho kitauziwa wakulimaa kwa bei nafuu..
Kando na kuwaokoa wakulima wa Kirinyaga kutokana na bei ya juu ya uzalishaaji wa mayai, kaunti hiyo pia inalenga kuwaepusha wakulima na vyakula ghushi.
Hivi karibuni Gavana Waiguru alianzisha mradi wa kuzalisha mayai milioni moja kwa mwezi na akawahakikishia wakulima kwamba watapata chakula bora cha kuku.
Tafsiri na Faustine Ngila
Alisema kwamba serikali yake itawapa chakula ya bure vikundi 32 ambavyo vinausika kwenye uzalishaji wa mayai.