• Nairobi
  • Last Updated May 16th, 2024 8:50 PM
Waiguru na madiwani hatimaye wakubali kushirikiana

Waiguru na madiwani hatimaye wakubali kushirikiana

Na George Munene

Gavana wa Kaunti ya Kirinyaga Anne Waiguru na madiwani wa kaunti hiyo ya wameamua kuzika tofauti zao na kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta maendeleo.

Walifanya makubaliano hayo Alhamisi baada ya mkutano mji wa Sagana.

Viogozi hao walisema kwamba waliamua kuzika tofauti zao ili wafanyie kazi wananchi wa Kirinyaga ambao wamekuwa wakiteseka kwa kukosa huduma muhimu.

“Tumeamua kuzika tofauti zetu ili tuhundumie wananchi  ambao walituchangua,” alisema Bi Waiguru.

Viogozi hao walisema kwamba barabara za kaunti hiyo ziko hali mbaya na zilikuwa zinahitaji kutengenezwa ili wananchi waweze kusafirisha mazao ya shambani sokono.

Walihahidi kurekebisha barabara ya kilomita 240 inayopita wenye maeneo ya ukulima chini ya miezi tano.

“Tutarekebisha barabara zote wadi zote,kazi ya ujezi wa barabara hizo itakamilika mwaka ujao,”alisema Bi Waiguru.

Viogozi hao walijutia mashindano yao ya kisiasa kwani yaliathiri maendeleo ya kaunti hiyo lakini waliwaakikishia mwananchi watafaidika na maridhiano hayo.

“Tuko tayari kuwafanyia kazi wananchi wa Kirinyanga kwani tumezika tofauti zetu,” alisema kiongozi wa wengi wa bunge la kaunti.

Tafsiri na Faustine Ngila

  • Tags

You can share this post!

Mwanaharakati aliye mstari wa mbele kuhakikisha mtoto wa...

RIZIKI: Mwalimu, mwokaji keki na mtengenezaji wa bidhaa za...