• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 6:47 PM
Waitaka serikali iwajibike vilivyo kuhifadhi mazingira

Waitaka serikali iwajibike vilivyo kuhifadhi mazingira

Na MAGDALENE WANJA

BAADHI ya wanamazingira wamemtaka Rais Uhuru Kenyatta kutangaza hali ya dharura ya mazingira nchini ili kuzuia kuzorota zaidi kwa mazingira.

Kulingana na wanamazingira hao, tangazo hilo litakuwa hatua muhimu katika kuokoa uridthi wa nchi ambao uko katika hatari ya kutokomea.

Wakiongozwa na Afisa Mkuu Mtendaji wa WildlifeDirect, Bi Paula Kahumbu, walisema kuwa kuzorota kwa mazingira kumechangia sana katika vifo vya wanyamapori na wale wa majini pamoja na miti hasa za kiasili.

Wanamazingira hao wametuma ombi kwa Rais kupitia barua iliyotiwa sahihi na wanamazingira wengine.

“Mito mingi imekauka, hali ambayo imesababisha kufa kwa samaki. Baadhi ya misitu pia imechomeka kwa muda wa miezi michache iliyopita na madharaka yake tayari yanaonekana,” inasema sehemu ya barua hiyo.

Kulingana na ripoti ya January 2019 UN Environment Foresight Brief, zaidi ya asilimia 40 ya wadudu wamepungua kwa kiasi kikubwa huku thuluthi moja wakiwa katika hatari kubwa.

Wadudu walioathirika sana ni pamoja na nyuki, vipepeo na siafu.

Licha ya Kenya kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki, bado kuna kiwango kikubwa cha takataka inayotupwa mitoni ikiwa ni zaidi ya tani 2,000 katika mito ya Nairobi pekee.

Walimtaka Rais kuunda jopo litakaloongoza na kusimamia utekelezaji wa maswala ya mazingira.

  • Tags

You can share this post!

‘Mwanamume mla kombamwiko’

Wanyama kwenye rada ya West Ham

adminleo