Habari Mseto

Wakataa barabara kupitia hifadhi ya wanyama pori

March 11th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

NA LUCAS BARASA

MASHIRIKA 73 ya watetezi wa kuhifadhi mazingira yamewasilisha ombi katika Jopo la Kitaifa la kutatua mizozo ya Mazingira yakitaka kusitishwa kwa ujenzi wa barabara inayopitia katika Hifadhi ya Kitaifa ya Aberdare.

Chini ya mwamvuli wa-The Conservation Alliance of Kenya (CAK), walitahadharisha kuwa barabara kuu inayopendekezwa ya Ndunyu Njeru – Ihithe itaathiri vibaya mfumo wa Ikolojia wa Aberdare.

“Sehemu hii ya mradi wa barabara ya Mau-Mau inaleta hatari kubwa na madhara yasiyoweza kurekebishwa kwa mfumo huu muhimu wa ikolojia,” makundi hayo yalisema katika taarifa iliyotolewa katika Hoteli ya Serena jijini Nairobi.

Mfumo wa ikolojia wa Aberdare, walisema, ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na ustawi.

Barabara hiyo itatatiza harakati za wanyamapori na wanaweza kugongwa na magari na kusababisha vifo na majeraha.

“Tumetoa tahadhari kwa serikali kuhusu athari za kimazingira za barabara inayopendekezwa

Wanasayansi kutoka vyuo vikuu vya Nairobi, Oxford, na Amsterdam, katika ripoti ya tathmini walionyesha kuwa barabara inayopendekezwa kupitia Hifadhi ya Misitu ya Aberdare na Mbuga ya Kitaifa “haitaleta watu karibu na lami”.