• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:42 PM
Wakazi wa Isiolo kupewa hatimiliki

Wakazi wa Isiolo kupewa hatimiliki

NA FAUSTINE NGILA

Zaidi ya wakazi 200 wa wadi ya Bulapesa mji wa Isiolo watapewa hatimiliki za ardhi zao huku serikali ya Gavana Mohamed Kuti ikitarajiwa kusajili vipande 4,000 kwenye mji huo.

Gavana Kuti alisema kwamba vyeti hivyo tayari vya vipande 294 vya ardhi ziko tayari na zitapeana mwezi huu.

“Tunataraji kupeana vyeti vya vipande 4000 ndani ya mji wa Isiolo na vyeti 294 vitapeanwa kati ya mwezi huu,” alisema Bw Kuti.

Alliongeza kuwa kupeanwa kwa vyeti hivyo kutahakikisha kwamba wakazi wana vipande vyao vya ardhi na kutatua mzozo ambao umekuepo wa ardhi.

Alisema kwamba watu tayari wameanza kujulishwa na kamati kaalum ya imeteuliwa kusaindia kuwatambua wamiliki wa ardhi.

Huku Isilolo ikishuhudia maendeleo mingi baada ya serikali ya ugatunzi lakini mizozo ya rdhi imekuwa ikirudisha nyuma ukuzi wa kaunti hio.

Maendeleo kama uwanja wa kimataifa wa Isiolo,Uwanja ,soko ya kisasa imevumia waekezaji huku bei ya ardhi ikipanda huku ikivutia wanyakuaji wa ardhi.

  • Tags

You can share this post!

Wauguzi Mandera waanza mgomo

2022: Wanasiasa wachochea mauaji