Habari Mseto

Wakazi wa Nairobi kupimwa corona bila malipo

October 16th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA FAUSTINE NGILA

Siku mbili zimetengwa mjini Nairobi watu kupimwa virusi vya corona bure huku kaunti hiyo ikijaribu kujiimarisha ili kubabiliana na janga hilo iwapo kutatokea maambukizi mapya.

Shughuli hilo litaendeshwa na mamalka ya Nairobi ya NMS kati ya Jumamosi Oktoba 17 na Jumapili 19 kwenye kaunti ndogo 17.

Hii itakuwa mara ya pili ya kaunti ya nNairobi kupima wananchi wake bila malipo mara ya kwanza shughuli hiyo lilifanyika mwezi May  ambapo Zaidi ya wananchi 3,000 walijitokeza kupimwa kwenye shugli hiyo iliyoendeshwa kwa sikiu 11.

Kaunti ya Nairobi na Mombasa ni kaunti ambazo zimeathirika sana na janga la corona tangu kisa cha kwanza kiripotiwe humu nchini mwezi Machi.

“Mamalaka ya Nairobi itakuwa ikipima wananchi kwenye kaunti ndogo zote Oktoba 17 na 18.”

Hii inajiri baada ya kushuhudiwa kwa kuongezeka kwa virusi vya corona baada ya Rais Uhuru Kenyatta kufungua uchumi.

Virusi vya corona vilikuwa vimepungua kwani visa 1,036 vimeripotiwa kati ya Septemba 22 na 27 lakini maambukizi yamendelea kuongezeka huku zaidi ya visa 300 vikiripotiwa.