• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Wakenya wa ughaibuni watuma hela nyingi kupiku matarajio

Wakenya wa ughaibuni watuma hela nyingi kupiku matarajio

Na BERNARDINE MUTANU

Kiwango cha fedha kilichowasilishwa nchini kutoka nje ya nchi mwezi wa Juni 2018 kwa mara ya kwanza kimepiku kiwango kilichowasilishwa Desemba 2017.

Kiwango hicho ni zaidi ya ilivyotarajia Benki Kuu (CBK). Katika ripoti ya hivi punde iliyotolewa na benki hiyo, wananchi wanaoishi nje ya nchi walituma Sh24.79 bilioni Desemba mwaka jana, ongezeko la asilimia 20 mwezi huo 2017.

“Pesa zilizotumwa kutoka Amerika Kaskazini zilikuwa ni asilimia 45, Ulaya 32 na kwingineko ulimwenguni asilimia 23 kiwango cha jumla cha fedha kilichotumwa Desemba 2018,” ilisema CBK.

Lakini mnamo Juni, kiwango hicho kilikuwa cha juu zaidi ikilinganishwa na Desemba ambapo jumla ya Sh27.08 bilioni zilitumwa nchini kulingana na CBK.

Ni mara ya kwanza tangu 2015 ambapo kiwango cha Desemba kimekuwa cha chini zaidi ikilinganishwa na miezi mingine.

  • Tags

You can share this post!

Waliostaafu kuhesabiwa tena kuondoa wale bandia

Deacons yatimua wafanyakazi 93 kubana matumizi

adminleo