• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 11:46 AM
Wakenya wabunifu kuwania Sh5 milioni

Wakenya wabunifu kuwania Sh5 milioni

Na BERNARDINE MUTANU

Ikiwa wewe ni mbunifu una nafasi ya kujishindia Sh5 milioni katika shindano la Johnson & Johnson.

Hii ni baada ya kampuni hiyo kuanzisha awamu ya pili ya Africa Innovation Challenge.

Wabunifu watawasilisha mawazo yao ya kibunifu katika sekta za afya na mazingira ambaye yanaweza kutekelezwa na kuzifaa jamii za Kiafrika.

Kulingana na afisa mkuu wa teknolojia wa Johnson & Johnson Josh Ghaim, mradi huo unalenga kutoa suluhu kwa changamoto ibuka.

“Lengo letu katika shindano hilo ni kukuza wawekezaji wa kanda hii kwa kutafuta suluhu za kibunifu katika masuala ya dharura,” alisema Bw Ghaim.

Maeneo yanayolengwa ni bustani, jinsi ya kupakia, afya ya kiakili, msaada kwa wahudumu wa afya, afya kwa njia ya kidijitali na huduma za upasuaji.

Watu kutoka kote barani wana nafasi ya kutuma maombi kibinafsi, makundi na kampuni kuambatana na mahitaji ya shindano hilo.

Siku ya mwisho ya kutuma maombi ni Januari 16.

  • Tags

You can share this post!

Mwanamke afichua kuvuta bangi kila siku kulimsaidia...

Walioiba mamilioni ya sacco kidijitali wanaswa

adminleo