Habari Mseto

Wakenya waishio Amerika wana bidii sana – Bloomberg

August 22nd, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na BERNARDINE MUTANU

RAIA wa Kenya wanaofanya kazi Marekani wameorodheshwa miongoni mwa wahamiaji walio na bidii zaidi humo.

Wakenya walipata asilimai 73.4, kuwa nambari tatu katika orodha ya wahamiaji walio na bidii zaidi marekani, na pia walio na ujuzi zaidi.

Ripoti hii ni kwa mujibu wa utafiti wa kampuni ya Bloomberg, 2018. Utafiti huo uliwaorodhesha raia wa Ghana wa kwanza na kufuatwa na waliotoka Bulgaria kwa kupata asilimia 75.2 na asilimia 74.2 kwa utaratibu huo.

Mataifa mengine yaliyotajwa katika utafiti huo ni Ethiopia (4), Misri (5), Nigeria (8) na Liberia (9).

Kwa jumla, Waafrika walipatikana kuwa na bidii zaidi wakilinganishwa na wahamiaji wengine, kwa mfano, kutoka Mexico na Central America, ambao ni zaidi ya asilimia 70 ya wahamiaji nchini humo.

Kulingana na ripoti hiyo, idadi ya Wakenya wanaoishi Marekani, na walio na kibali ni 120,000.