• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 12:45 AM
Walimu 15 kuzuiliwa kuhusiana na wizi wa KCSE

Walimu 15 kuzuiliwa kuhusiana na wizi wa KCSE

Na JADSON GICHANA

Walimu 15 Jumanne walifikishwa katika mahakama ya Kisii kwa kosa la kupatikana na maswali ya mtihani wa KCSE kinyume cha sheria.

Washukiwa hao ni pamoja na Naibu wa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Monianku, Msimamizi wa mtihani huo na walimu wasaidizi katika usimamizi huo.

Kumi na tano hao walifikishwa mbele ya Hakimu Mkaazi, Margret Nafula ambapo walikabiliwa na mashtaka matatu ya kupatikana na karatasi hizo.

Walimu hao ni pamoja na Irene Kivunja, Judith Nyaboke, Marori Edwin, Alex Ziko, Chrispers Ogora, Abuta John waliopatikana na karatasi ya KCSE 233/1 ya Kemia Novemba 5, 2018 katika shule ya Sekondari ya Monianku, Kaunti ndogo ya Gucha, Kaunti ya Kisii kinyume cha sheria.

Katika shtaka la pili Motende John, Abuta John, Benard Omworo, Omgwa Joel Joel nyakwanya Gedion Nyagaka, Edna Bitutu, Peter Arori Chritopher Otieno na Ann Nyaboke walipatikana wakiwa wanamiliki mtihani huo kinyume na sheria za Baraza la Mitihani nchini (KNEC) 2012 katika kipengele 27(3).

Shtaka la tatu Irene Kivunja, Judith Nyaboke, Marori Edwin, Alex Ziko, Chrispers Ogora, Abuta John, Peter Arori, Christopher Otieno na Judith Nyaboke walishtakiwa kwa kusaidia katika wizi huo kinyume cha sheria katika Baraza la usimamizi wa mtihani (KNEC) 2012 sehemu 40.

Mnamo Novemba 5, 2018 katika shule ya Sekondari ya Monianku, Kaunti ndogo ya Gucha, Kaunti ya Kisii kwa pamoja wanadaiwa kutenda kitendo hicho kwa kujaza majibu kwenye karatasi hiyo ya mtihani wa KCSE Kemia (1).

Pia, wawili walitoroka na wanatafutwa na maafisa wa usalama.

Walifikishwa mbele ya Hakimu Mkaazi, Margret Nafula walikabiliwa na mashtaka matatu ya kupatikana na karatasi hiyo nje ya shule katika boma moja.

Upande wa mashtaka uliomba mahakama hiyo kuwazuilia katika kituo cha Polisi cha Nyamarambe hadi uchunguzi ukamilike.

You can share this post!

Raila kukutana na madiwani kumaliza mzozo wa uongozi

ODM yapuuzilia mbali ziara ya Ruto

adminleo