• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 5:50 AM
Waliobwagwa 2017 wasubiri kujaribu bahati 2022 – Waititu

Waliobwagwa 2017 wasubiri kujaribu bahati 2022 – Waititu

Na LAWRENCE ONGARO

VIONGOZI walioshindwa uchaguzini wanastahili kuketi kando na kuachia waliochaguliwa kuendesha maendeleo.

Gavana wa Kiambu Bw Ferdinand Waititu, alisema mahasidi wake wengi wamejaribu kumdunisha kama asiye na masomo, lakini yeye hatatishwa na matamshi hayo.

“Kuna wengine wamenihusisha na ufisadi lakini iwapo watazuru maeneo tofauti katika Kaunti ya Kiambu, watapata miradi mingi yamekamilika huku mengine yakiendelea kukamilishwa.

Aliyasema hayo Jumamosi eneo la Juja wakati wa uzinduzi wa kufungua afisi mpya ya naibu wa Kamishna wa Kaunti ndogo ya Juja, iliyogharimu takribani Sh 30 milioni.

Alisema tayari amewasiliana na wakili wake ili kuishtaki kituo kimojacha runinga kwa kuiharibia jina kaunti hiyo kuhusu ufisadi.

“Kabla ya kutangaza mambo ni vyema kufanya uchunguzi kamili. Sijui watu hawa walipata wapi ripoti eti afisa mmoja wangu alipatikana na mamilioni ya fedha katika gari lake. Hayo najua ni maneno ya kusingizia na nitalazimika kuwasilisha malalamiko yangu mahakamani,” alisema Bw Waititu.

Alisema kwa muda wa miaka miwili unusu ambayo amekuwa uongozini miradi mingi imetekelezwa,kama ujenzi wa masoko, barabara, hospitali na madaraja.

Licha ya maadui wake fulani kueneza uvumi eti hata kuandika vyema hawezi na hata hana masomo ya kutosha, alieleza anafahamu vyema alijisajili katika Chuo cha Punjab India.

Baada ya afisi hiyokufunguliwa rasmi alisema hivi karibuni kutakuwa na zoezi la kuhesabu wafanyi kazi wote wa kaunti ili kuwa na idadi kamili wanaostahili kuwa huko.

Alisema kuna miradi mingi muhimu zinazowanufaisha wakazi wa Kiambu kama ujenzi wa masoko mapya yanayokaribia kukamilika maeneo ya Ruiru, Juja, Kikuyu, na Gachie.

Alisema kwa sababu kaunti ndogo ya Juja lina vijana wengi wasio na ajira amependekeza chuo cha mafunzo cha Polytechnic lijengwe ili vijana waweze kupata nafasi ya kupata masomo ya kiufundi.

“Ninataka kuona vijana wakijitafutia riziki bila kuhangaishwa na yeyote, na hata wanawake wanaoendesha biashara zao mitaani hawastahili kusumbuliwa na yeyote,” alisema Bw Waititu.

Alitoa onyo kali kwa wafanyi kazi wazembe ambao hawatekelezi wajibu wao kuwa hatawasaza bali watapigwa kalamu bila huruma.

Alizidi kueleza ya kwamba atafanya juhudi kama gavana wa Kiambu kuona ya kwamba wakazi wapatao 1.2 milioni wanapata huduma bila kubagua yeyote.

You can share this post!

‘Maeneo kame yanaweza kugeuzwa ya uzalishaji...

Kuria sasa asajili TNA

adminleo