• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
Waliomuua mwalimu wasakwa

Waliomuua mwalimu wasakwa

SHABAN MAKOKHA NA FAUSTINE NGILA

Polisi wanatafuta majambazi ambao walimteka nyara mwalimu mmoja wa shule ya upili kutoka nyumbani kwake Shinoyi kaunti ndogo ya Navakolo na kumuua kilomita kadhaa kutoka kwake Jumatano.

Iliibuka kwamba Bw Ernest Opondo mwenye miaka 54 alikuwa tayari ameruka kutoka kwa gari la watekaji hao na kujifungia ndani ya nyumba iliyokuwa karibu kwenye barabara ya Ekero-Butere lakini wahuni hao wakamfuata na kumuua nyumbani kwa Hamisa Malala saa tano na nusu asubuhi.

Mkuu wa DCI Kakamega Robeert Muriithi alisema kwamba walitambua mwenye gari hilo ambalo lilitumika katika kumteka nyara mwalimua huyo.

Mwathiriwa alipigwa risasi mara mbili. Alisema kwamba sababu ya kuuliwahawaijui lakini familia ilisema kwamba ilikuwa ni maswala yanayohusiana na mizozo ya ardhi.

“Tumechukua vidole vyao na tunashirikiana na NTSA kutafuta gari hio iliyotumika na waalifu hao yenye usajili wa KCS 503L,”alisema Bw Murithi.

“Tunachukua habari kutoka kwa watu tofauti akiwemo babake na ndunguye ambao wanasemekana kuwa walikuwa na mzozo na mwalimu huyo kabla ya kifo chake.”Mwalimu huyo alichukuliwa na majagili hao kutoka nyumbani kwake.

Kulingana na mke wake Maurine Atema mwalimu wa shule ya upili sule ya wasichana ya Lirhanda majangili hao walikuwa na mazungumzo na bwanake kabla ya kumteka nyara.

Walimweka kwenye buti ya gari ndogo alioegesha nje ya boma lao. Baada ya kupokea habari hizo wanakijiji walivamia nyumba ya nduguye Bw Calistus Weremba na kuchoma nyumba yake.

Baadaye walivamia nyumbani kwa babake na kuchukua ng’ombe watatu ambao walichomwa.

  • Tags

You can share this post!

Familia ya muuguzi wa Homa Bay yataka ifidiwe

Wawili waliomuua mteja wa M-Pesa watafutwa