Walioshtakiwa kununua rukwama za Sh900,000 warudishwa ndani
Na RICHARD MUNGUTI
KUHUKUMIWA kwa waliokuwa wafanyakazi wa kaunti ya Bungoma waliopatikana na hatia ya kununua rukwama tisa kwa gharama ya Sh983,880 kuliahirishwa kwa mara ya nne Ijumaa baada ya hakimu kusemekana ni mgonjwa.
Kutosomwa kwa hukumu hii iliyokuwa imesubiriwa kwa hamu na ghamu kuliimbua manung’uniko makali kutoka kwa familia za washtakiwa hata ikabidi hakimu aamuru wanyamaze na kuheshimu korti.
Adhabu ilikuwa inatarajiwa kupitishwa na hakimu mkuu wa Kakamega Bw Bildad Ochieng’.
Kesi hiyo ilitajwa mbele ya hakimu mwandamizi Bw Thomas Muraguri aliyewajulisha washtakiwa kuwa Bw Ochieng’ hajihisi vizuri na hakufika kortini.
“Hakimu aliyesikiza kesi hii hajisikii vizuri. Hakufika kazini leo. Itabidi kesi hii itajwe Juni 25 2018 ,” alisema Bw Muraguri.
Alipoahirisha kusomwa kwa uamuzi huo Bw Ochieng’ alisema hakuwa ametayarisha uamuzi huo kutokana na kazi nyingi.
Lakini nje ya mahakama kulikuwa na sokomoko huku washtakiwa wakiwapungia mikono jamaa wao huku wakisukumwa kuingia seli na maafisa wa polisi.
Baadhi ya jamaa wa washtakiwa waliwaambia wajipe moyo vita vinaendelea (Aluta Continua).
Washtakiwa hao walipatikana na hatia ya kufuja pesa za umma kwa kununua Wilubaro tisa kwa bei ya ShSh 983,880, kumaanisha kila moja ilinunuliwa kwa bei ya Sh109,350.
Walioshtakiwa ni Bw Howard Lukadilu (mwenyekiti wa kamati ya utoaji zabuni), Bw Oscar Onyango Ojwang’ (naibu wa mwenyekiti) na Bw John Juma Matsanza (afisa mkuu).
Wengine walioshtakiwa ni Ayub Tuvaka China, Arlington Shikuku Omushieni, Jacquueline Nanjala Namukali na Reuben Cheruyiot Rutto.
Upande wa mashtaka unaoongozwa na Bw Paul Juma uliomba korti iwasukumie kifungo cha miaka 10 gerezani akisema makosa waliyoyafanya ni mabaya