• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 2:00 PM
Wanafunzi 3,000 walihepa kufanya KCSE 2023 licha ya kujisajili – Wizara

Wanafunzi 3,000 walihepa kufanya KCSE 2023 licha ya kujisajili – Wizara

NA MWANGI MUIRURI 

RAIS William Ruto ameidhinisha kuachiliwa kwa matokeo ya Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE 2023), ikiibuka kwamba wanafunzi 3,000 hawatapata matokeo yao.

Hii ni baada ya Rais kuelezewa na Waziri wa Elimu Bw Ezekiel Machogu kwamba licha ya kusajiliwa, wanafunzi hao hawakushiriki zoezi la kufanya mitihani.

Rais pia ameamrisha wizara ya elimu iadhibu vikali visa vyote vya udanganyifu ili kuipa sekta ya elimu uadilifu na imani katika jumuia ya wasomi huku mataifa kadha yakielezea wasiwasi wao na utapeli wa hati za elimu hapa nchini.

Baada ya kupewa idhini hiyo, waziri Machogu na wadau ndio kwa sasa wanaachilia matokeo hayo wakiwa katika Kaunti ya Uasin Gishu, Shule ya Upili ya Moi Girls Eldoret.

  • Tags

You can share this post!

Askofu Kimengich amshauri Ruto kupunguza makali yake kwa...

Usajili wa watahiniwa wa KPSEA na KCSE 2024 kuanza Januari...

T L