Wanafunzi 55,000 wa shule za kibinafsi gizani
NA VITALIS KIMUTAI
Wanafunzi 55,000 wa shule za kibinafsi hawajui watakapoenda baada ya shule zao kukosa kufunguliwa Jumatatu.
Maelfu ya wanafunzi wa Darasa la Nne, la Nane na Kidato cha Nne watalazimika kutafuta shule zingine.
Kwa sasa zaidi ya shule za kibinafsi 200 na sekondari zimefungwa huku wenyewe wakizigeuza kuwa maeneo ya biashara ama kushindwa kulipa kodi huku mwenye nyumba wakizichukua.
Shule ya kibinafsi ya Whistling Thorn Kawangware ni kati ya shule mabazo wenyewe wamezifanya kuwa nyumba za kukodisha
Afisa wa muungano wa shule za kibinafsi Peter Ndoro aliambia Taifa Leo kwamba shule 207 hazikufunguliwa.
“Idadi hiyo inaweza kuwa kubwa kwani si shule zote ni washiriki wa chama chetu,” alisema.
Wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mtihani wa kitaifa watalazimika kufanyia mtihani shule zingine.
TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA