• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 2:58 PM
Wanafunzi waonyesha umahiri wao katika tamasha za muziki

Wanafunzi waonyesha umahiri wao katika tamasha za muziki

Na ANTHONY NJAGI

TAMASHA za 93 za muziki ziliingia siku yake ya pili Jumapili katika Chuo Kikuu cha Kabarak, huku wanafunzi wa chekechea, shule za msingi na vyuo wakijitosa jukwaani kuonyesha talanta zao.

Mashindano hayo ambayo yamesifiwa kuwa ya kipekee eneo la Afrika Mashariki na ya Kati, yaliongozwa na Mkurugenzi wa Elimu Rify Valley, Bw John Ololtuaa, likihudhuriwa na walimu pamoja na umma.

Wanafunzi wa shule ya wavulana ya Ndere kutoka Nyanza ndio waliibuka washindi katika shindano la wimbo wa jumuiya ya Afrika Mashariki, wakifuatwa na wale wa shule ya Esirisia kutoka Magharibi na shule ya msingi ya Thika ya watoto wenye ulemavu wa macho.

Katika shindano la nyimbo za Kiafrika, wanafunzi wa shule ya msingi ya Booker waliibuka washindi, wakifuatwa na wale wa shule ya msingi ya Moi Kabarak, nao wa shule ya msingi ya Tabor wakaibuka nambari tatu.

Katika shindano la nyimbo, shule ya St Paul’s Educational Centre- iliibuka nambari moja, ikafuatwa na Karatina DEB, kisha shule ya msingi ya Imani kutoka Bonde la Ufa.

Wanafunzi wa madarasa ya juu katika shule za msingi walitumbuiza hadhira kwa nyimbo za Kiafrika na za Kizungu.

You can share this post!

Ripoti ya BBI kutayarishwa kuanzia leo, Haji atangaza

Spika awashauri magavana kuandaa manaibu kuongoza

adminleo