• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 11:53 AM
Wanahabari wajitokeza kwa wingi kumzika mwenzao aliyefariki

Wanahabari wajitokeza kwa wingi kumzika mwenzao aliyefariki

Na LAWRENCE ONGARO

WANANCHI wamehimizwa kuchukua jukumu la kukaguliwa afya kama njia ya mapema ya kuzuia matatizo mbalimbali ya kiafya.

Ni wito uliotolewa na wataalam wa afya waliohudhuria mazishi ya afisa mkuu wa habari wa Kenya News Agency (KNA) kaunti ndogo ya Thika Bi Lucy Njeri Njoroge aliyefariki majuzi baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Mazishi yake yalifanyika mnamo Ijumaa katika kijiji cha Mutunguru, Gatundu Kusini.

Marehemu amemwacha mumewe Bw Peter Njoroge Waruiru na watoto watatu ambao in Victoria Wambui, Jacqueline Nyawira, na Jaycob Waruiru.

Marehemu wakati akiwa hai alikuwa akijishughulisha na maswala ya uandaaji wa habari kwa muda si chini ya miaka 27 huku akihudumu zaidi ya miaka minane eneo la Thika.

Baadhi ya maeneo aliyofanyia kazi wakati wa kuendeleza taaluma yake ya uandishi ni Kirinyaga, Embu, Nyeri, na, Thika.

Mazishi hayo yalihudhuriwa na  maafisa wakuu wa KNA kutoka Nairobi, maafisa wakuu wa serikali na marafiki wengi kutoka maeneo tofauti kote nchini.

Njia ya kipekee

Waandishi wa habari kutoka Thika na Kiambu wapatao 25 walimsindikiza mmoja wao kwa njia ya kipekee huku wakimwimbia wimbo maalum wa Sauti Soul uitwao ‘Safiri Salama’.

Ibada ya mazishi iliendeshwa kwa njia ya kipekee na Askofu mkuu wa kanisa la Living Faith Ministry (LFM), Askofu Jack Kamere huku akiendesha mahubiri yake kutoka kitabu cha Pslams 91:1-2.

Aliwahimiza Wakristo kujiandaa kwa kifo kwa sababu ukifanikiwa kuingia mbiguni, hutakumbana na shida za dunia tena.

Wakristo pia walihimizwa kuzuru hospitality kila Mara hata Mara mbili kwa mwaka ili kujua hali ya Afya yao.

“Kile kinachodhuru afya zetu in kwenda kwa daktari dakika za mwisho huku ikiwa in vigumu kukabiliana na maradhi yaliyoenea zaidi mwilini,” alisema mmoja wa wataalamu wa kiafya aliyehudhuria hafla hiyo.

  • Tags

You can share this post!

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Nafasi na mchango wa lugha...

Young Dragon Karate Club yazidi kujituma

adminleo