• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Wanaoshukiwa kumteka nyara Mwitaliano kusalia ndani

Wanaoshukiwa kumteka nyara Mwitaliano kusalia ndani

Na RICHARD MUNGUTI

WASHUKIWA watatu wanaodhaniwa walihusika na utekaji nyara wa raia wa Italia  Bi Silvia Constanza Romano mjini Malindi kaunti ya Kilifi watasalia korokoroni kwa muda wa siku 30 kuwasaidia polisi kubaini aliko.

Mabw Mohamed Abdirahman Abdile, Aden Hassan Mohamed na  Ibrahim Ali Bayow  walikifishwa mbele ya hakimu mwandamizi Bi Martha Mutuku aliyewaruhusu polisi waendelee kuwazuilia washukiwa hao.

Kwa mujibu wa maafisa wa polisi wa kupambana na ugaidi watatu hao wanaoelewa tu lugha ya Kisomali walitiwa nguvuni mjini Garissa wiki iliyopita wakiwa na bunduki bila vyeti vya kumiliki.

Mahakama ilijulishwa Abdile aliwasaidia washukiwa hao wengine wawili Mohamed na Bayow kuingia humu nchini kutoka Somalia.

“Uchunguzi uliofanywa umebaini huenda walihusika na utekaji nyara wa Bi Romano.

Mahakama ilielezwa kuwa watatu hao wako na uhusiano na washukiwa wengine wanaoendelea kusakwa na Polisi.

Zaidi ya watu 100 wametiwa nguvuni kaunti za Kilifi na Tana River tangu kutekwa nyara kwa Romano.

“Taarifa za kijasusi zaeleza kuwa washukiwa hao na washirika wenzao walipanga njama za kumteka nyara mfadhili huyo na kwamba ipo haja ya kuwazuilia saiku 30 hadi uchunguzi ukamilishwe,” alisema afisa anayechunguza kesi hiyo Bw Vitalis Kibet.

Bi Romani alitekwa nyara mnamo Novemba 20 2018 mwendo wa saa moja unusu jioni katika kijiji cha Chakama , mjini Malindi na washukiwa wanaodhaniwa kuwa magaidi wa Al Shabaab

  • Tags

You can share this post!

Washukiwa wa shambulizi la Garissa kujitetea Machi 21

TANZIA: Oliver Mtukudzi alivyotambulika kimataifa

adminleo