• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 8:22 PM
Wanasiasa waonywa dhidi ya kuzua ghasia mazishini

Wanasiasa waonywa dhidi ya kuzua ghasia mazishini

NA SHABAN MAKOKHA

WANASIASA kutoka eneo la Magharibi mwa Kenya, wameonywa dhidi ya kuzua ghasia katika hafla za mazishi na kunyima familia za wafiwa fursa kuaga wapendwa wao kwa heshima.

Katika eneo la Magharibi na Nyanza, wanasiasa wanatumia mazishi kuzua taharuki wakijaribu kuonyesha ushawishi wao kwa waombolezaji wakilumbana na wakati mwingine wanapigana hadharani na kuvuruga hafla hizo.

Familia nyingi huwa zinapata hasara na madeni baada ya viti vya kukodisha, mahema na magari kuharibiwa na hata chakula kuibwa.

Visa vya hivi punde vilitokea Jumamosi, Machi 23, 2023 eneo la Matungu, Kakamega na Goseta, Trans Nzoia ambapo waombolezaji walilazimika kutimua mbio na watu wa familia wakaondoa miili ya wapendwa wao baada ya makundi yanayounga wanasiasa tofauti kupigana.

Kisa cha Trans Nzoia, kilishirikisha wafuasi wa Gavana wa Kaunti hiyo, Bw George Natembeya na wale wa Spika wa Bunge la Kitaifa, Bw Moses Wetangula.

Aidha, familia iliyofiwa, ililazimika kuzika mpendwa wao bila kufuata kanuni, mila na tamaduni zao kwa hofu ya mashambulizi zaidi.

Matukio haya yalijiri baada ya Waziri wa Usalama wa Ndani Prof Kindiki Kithure kuonya wanasiasa dhidi ya kutumia wahuni kuvuruga hafla za mazishi.

Waziri alisema hakuna aliye juu ya sheria na yeyote anayezua ghasia katika hafla za umma atachukuliwa hatua za kisheria.

 

  • Tags

You can share this post!

Mbinu kudumisha mahusiano ya ‘mali’  

Rachel Ruto: Serikali itabuni kikosi kuombea polisi...

T L