Wasiwasi Busia familia zikiendelea kupata watoto wafupi
WAZAZI Kaunti ya Busia wana wasiwasi kuhusu ongezeko la idadi ya watoto walio na ukuaji uliodumaa.
Haya yanajiri kufuatia ufichuzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa ya Kuhudumia Watoto (UNICEF) unaoonyesha kuwa asilimia 15 ya watoto katika Kaunti ya Busia wanakabiliwa na tatizo hilo.
Kulingana na takwimu rasmi za UNICEF, idadi kubwa ya watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano Busia, wanakabiliwa na ukuaji uliodumaa.
Bw Gerald Ochieng kutoka kaunti ndogo ya Matayos alisema mwanawe mwenye umri wa miaka 15 amedumaa na kuwa ana urefu wa futi tatu.
“Familia yetu na ya mke wangu inajumuisha watu warefu kwa wastani. Lakini mwanangu aliyezaliwa 2020 haonyeshi dalili za kukua,” alisema Bw Ochieng.
Naye Richard Ojuma kutoka Kakapel, Teso Kaskazini anasema kuwa watoto wake watatu wa miaka 20, 17 na 15 ni wafupi na hawaonyeshi dalili yoyote ya kukua zaidi.
Bw Ojuma na mkewe Joyce wanatoka katika familia za watu warefu.
“Nina wasiwasi. Hii inaweza kusababisha kizazi cha watoto wafupi kama ilivyokuwa Kongo,” alisema Bw Ojuma.
Ripoti ya UNICEF inaashiria lishe duni kama sababu kuu ya tatizo hilo miongoni mwa watoto huko Busia