• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 5:50 PM
Wasiwasi usherati ukichacha katika kambi ya waathiriwa wa mafuriko

Wasiwasi usherati ukichacha katika kambi ya waathiriwa wa mafuriko

SHABAN MAKOKHA NA VICTOR RABALLA

WAATHIRIWA wa mafuriko katika eneo la Bunyala, Kaunti ya Busia, wamelalamikia ongezeko la vitendo vya uasherati katika kambi za muda wanakokaa, zilizo katika shule tofauti tofauti.

Wanandoa wanalalamika kukosa pahala pa kushiriki mchezo wa huba na wenzao, kutokana na ukosefu wa mazingira mwafaka wa kufanyia kitendo hicho.

Zaidi ya familia 600 zimeachwa bila makao kutokana na mafuriko katika kaunti hiyo.

Wasichana wadogo wamekuwa wakilalamika dhidi ya kunyanyaswa kingono na wanaume wa umri mkubwa.

Wanasema wanahofia kwamba huenda kushiriki vitendo hivyo kukawaletea mimba za mapema.

Wanandoa wamekuwa wakilalamika kukosa kufanya tendo la ndoa kwa muda mrefu, kwani wamekuwa wakilazimika kulala katika vyumba sawa na watoto wao.

“Tunapitia hali ngumu sana katika kambi hizi. Wanaume wakubwa wanatusumbua kimapenzi. Wengi wetu tutatoka katika kambi hizi tukiwa na watoto,” akasema mmoja wa wasichana katika kambi hizo.

Bw James Matheri alisema masuala hayo yamegeuka kuwa tatizo kubwa kwa familia nyingi, na huenda yakachangia baadhi yazo kuvurugika.

“Wakati wanandoa waliooana wanakabiliwa na hali ngumu kupata mahali mwafaka pa kushiriki ngono katika kambi hizo, baadhi yao wanajihusisha na uasherati na watu wengine katika kambi hizo. Kuna mambo mengi yanayoendelea,” akasema Bw Matheri.

Watu kutoka familia tofauti wanalala katika madarasa sawa na watoto wao na majirani.

Wakati huo huo, waathiriwa wa mafuriko katika eneo la Nyando, Kaunti ya Kisumu, wanaomba kupewa misaada ya dharura, kwani hali ya kibinadamu katika eneo hilo imedorora.

Naibu Chifu wa eneo hilo, Bw Neto Ong’udi, alisema kuwa familia 500 zinakabiliwa na hatari ya kukumbwa na njaa, baada ya karibu ekari 450 za mashamba yaliyokuwa na mazao kukumbwa na mafuriko.

  • Tags

You can share this post!

Spika wa Bunge aliyeanza maisha kama ‘beach boy’

Tunda la peazi ni nadra sokoni lakini ukilipata,...

T L