• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 8:03 AM
Watu 80 kukamatwa kwa kususia vikao vya korti

Watu 80 kukamatwa kwa kususia vikao vya korti

Na Titus Ominde

Mahakama ya Eldoret ilitoa ilani ya kukamatwa kwa watu wapatao 80 ambao wamekuwa na mazoea ya kukwepa korti kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita.

Hakimu mkuu wa Eldoret Bw Charles Obulutsa alisema washtakiwa lengwa ni wale ambao waliachiliwa kwa dhamana.

Akihutubu alipokuwa akiwahutubia wana kamati wa kamati ya watumiaji mahakama mjini Eldoret (CUC) Bw Obulutsa alionya washtakiwa ambao wameachiliwa kwa bondi dhidi ya kukosa kuhudhuria vikao vya mahakama wanapohitajika.

Hakimu Obulutsa alisema tabia ya washtakiwa kukosa kuhudhuria kesi zao wanapohitajika kufanya hivyo imechangia pakubwa kwa mirundiko ya kesi mahakamani hasa kesi za uhalifu.

“Sisi kama mahakama tunajaribu kadri ya uwezo wetu kukabiliana na mirundiko ya kesi changamoto hutokea wakati washtakiwa ambao wameachiliwa kwa bondi wanapokosa kufika mahakamani,” alismea Bw Obulutsa

Hakimu huyo alisema bondi ya watu kama hao itatwaliwa na serikali kwa mujibu wa sheria.

Vile vile hakimu huyo alionya wadhamini wa dhamana husika kuwa watakamatwa na kuzuiliwa iwapo watu ambao wanadhamini watakosa kufika mahakamani kwa mujibu wa maagizo ya mahakama.

Wakati huo huo kamati ya CUC mjini humo ilipongeza idara ya polisi kwa kukabiliana na tabia ya kupotea kwa faili za mahaka mara kwa mara.

Kamati hiyo iliseme tangu idara ya polisi ikumbatie marekebisho tabia hiyo imepungua kwa kiasi kikubwa.

  • Tags

You can share this post!

Kericho, Bomet kufikishwa kortini kwa kuhudumu bila...

Makasisi wa ACK waliofutwa kulipwa Sh6.8 milioni

adminleo