Habari Mseto

Wavuvi walia maji kuzamisha biashara ya samaki

October 7th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA SAMMY LUTTA

Zaidi ya wanakijiji 200,000 ambao wanategemea uvuvi katika Ziwa Turkana wanakondolea macho baa  la njaa kwasababu ya kuongezeka kwa maji kwa ziwa hilo na kufunika ufuo.

Wavuvi hao wanakadiria hasara ya mamilioni kwani maji yameongezeka kwa zaidi ya kilomita moja na kufunika ufuo, hali inayozua neti na mashua kubebwwa na maji.

Bi Nachere alisema kwamba hasara hiyo iliathiri wavuvi wadi ambazo ziko karibu na ufuo wa ziwa hilo Lakezone Keri Delta, Kangatotha na Kalokol.

“Maeneo ya kuhifadhi samaki yanayomilikiwa na usimamizi wa ufuo wa Todonyang na Lowarengeak yote yamejaa maji. Biashara ya samaki imeathiriwa sana,” alisema.

Maeneo ya ufuo ya Lomekwi, Katiko, Kataboi, Nasechabuin na Kalimapus yameathirika pia na uongezeka la maji.

“Wavuvi wengi wanahofia kukabiliwa na mamba alisema,” Mr Peter Nang’ori  huku akiomba wasaidiwe na msaada wa chakula.

 

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA