Habari Mseto
Waziri Murkomen, Kositany wanusurika katika ajali ya ndege

Waziri wa Barabara na Uchukuzi Kipchumba Murkomen (kushoto) na mwenyekiti wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (KAA) Caleb Kositany. PICHA | MAKTABA
NA MWANDISHI WETU
HELIKOPTA iliyombeba Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen na mwenyekiti wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (KAA) Caleb Kositany imeanguka ikitaka kupaa wakitoka Baringo kuenda kuhudhuria mazishi ya mamake Mkurugenzi Mtendaji wa KAA.
Hakuna majeruhi.
Afisi ya waziri Murkomen imethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.