• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 3:09 PM
Wenye hela kugharimia mawasiliano ya wasiojaliwa kiuchumi Safaricom

Wenye hela kugharimia mawasiliano ya wasiojaliwa kiuchumi Safaricom

Na PETER MBURU

KAMPUNI ya mawasiliano ya simu Safaricom imetangaza kuwa siku zijazo wateja wake wataweza kupiga simu bila kuwa na hela za muda wa maongezi , lakini kwa kumsukumia anayepigiwa gharama ya kupiga simu.

Katika huduma hiyo, mtu anayetaka kumpigia mwingine simu ilhali hana pesa atakuwa akibonyeza alama ya reli (#) katika simu yake kabla ya nambari ya anayempigia, kisha kuanza kupiga.

Anayepigiwa naye baada ya kupokea simu atasikia sauti itakayomtaka kubonyeza ‘1’ ili waendelee kuzungumza na anayempigia. Pesa za anayepigiwa ndizo zitatumika wakizungumza kwa namna hiyo.

“Tunataka kuwapa wateja wetu huduma zinazofaa na wanazohitaji. Uzinduzi huu unalenga kuhakikisha wateja wetu wanaendelea kushikana na wapendwa wao,” akasema afisa mkuu wa huduma za wateja Safaricom Bi Sylvia Mulinge.

Huduma hiyo imezinduliwa kusaidiana na ile ya “Please call me” ambayo Wakenya wengi wasio na pesa huitumia, kumtaka mtu wanayemtafuta kuwapigia.

You can share this post!

Uhuru sasa aonywa kuhusu uwezo wake kiushawishi Mlima Kenya

Ruto aahidi kutatua mzozo wa wabunge na maseneta

adminleo