DCI washtaki Boniface Mwangi kwa kumpata na mikebe ya vitoa machozi, kasha tupu la risasi
MWANAHARAKATI Boniface Mwangi amekanusha mashtaka ya kupatikana na mikebe miwili ya vitoa machozi na kasha tupu la risasi.
Alipofikishwa mbele ya mahakama ya Kahawa Jumatatu, Julai 21, 2025, Mwangi ambaye alioneka mtulivu baada ya kuzuiliwa seli kwa siku mbili, alikanusha mashtaka hayo mawili huku mawakili wake wakiongozwa na Martha Karua wakiitaka mahakama imwachilie kwa dhamana ya Sh5,000 wakisema hakuna sababu za maana za kuendelea kumzuilia.
Polisi wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) walisema wapata silaha hizo walipofanya upekuzi katika afisi zake za Mageuzi Hub, Nairobi.
Mahakama iliamuru Mwangi kuachiliwa kwa dhamana ya kibinafsi ya Sh1 milioni na kuagiza kesi hiyo itajwe Agosti 19 kwa maelekezo zaidi.